IQNA

Wanafunzi Wakristo Zimbabwe wajifunza kuhusu Uislamu

9:56 - August 09, 2016
Habari ID: 3470510
Wanafunzi Wakristo nchini Zimbabwe wameshiriki katika warsha ya siku moja kuhusu Uislamu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, warsha hiyo imeandaliwa na Mwambata wa Utamaduni wa Iran mjini Harare.

Zimbabwe ni nchi ambayo wakaazi wake wengi ni Wakristo na hivyo imeathiriwa vibaya na wimbi la chuko dhidi ya Uislamu au Islamophobia. Hali hiyo imekuwa mbaya zaidi kutokana na kuenea makundi ya magaidi wakufurishaji wenye misimamo mikali barani Afrika kama vile Boko Haram na Al Shabab.

Idara ya Utamaduni ya Iran nchini Zimbabwe imechukua hatua za kupunguza athari mbaya za chuki dhidi ya Uislamu na moja ya nchi hiyo ni kuandaa warsha ya kuujua Uislamu ambapo wanafunzi Wakristo wamepata mafunzi katika Msikiti wa Aal Muhammad mjini Harare.

Warsha hiyo imeendesha kwa msaada wa Sheikh Mahdi, mwanazuoni wa Kiislamu kutoka Iran aliye nchini Zimbabwe ambapo wanafunzi wakristo wamejumuika na wenzao Waislamu kutoka Chuo cha Fatima Zahra SA kujadili maudhui saba za Kiislamu katika mazungira ya kirafiki.

3521212


Washiriki wamejifunza kuhusu masuala kama vile sala, istilahi za Kiislamu, chakula halali, sawm, Bibi Maryam AS na Nabii Issa AS katika Uislamu, Hijabu na itikadi za Kiislamu.


Wanafunzi Wakristo Zimbabwe wajifunza kuhusu Uislamu

Wanafunzi Wakristo Zimbabwe wajifunza kuhusu Uislamu

captcha