IQNA

Milango ya misikiti kufungwa wakati wa Sala Uholanzi

10:49 - February 01, 2017
Habari ID: 3470828
IQNA: Kufuata hofu za hujuma za wenye chuki dhidi ya Uislamu, misikiti minne mikubwa nchini Uholanzi itafungwa wakati wa sala baada ya Waislamu sita kuuawa Canada walipokuwa wakiswali msikitini.







Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, uamuzi huo umechukuliwa na kamati za misikiti nchini Uholanzi, kufuatia hujuma ya kigaidi iliyopelekea Waislamu sita kuuawa na wengine kujeruhiwa walipokuwa wakiswali Sala ya Ishaa katika msikiti mmoja huko Quebec nchini Canada.

Katika taarifa ya pamoja, wasimamizi wa misikiti ya Msikiti wa Samawati mjini Amsterdam, as-Msikiti wa Ahul Sunnah The Hague's, Msikiti wa Essalam mjini Rotterdam na Msikiti wa Omar Al Farouq huko Utrecht wamesema misikiti hiyo wakati wa Sala kwa ajili ya usalama.Misikiti hiyo huwa na maelefu ya waumini kila siku.

Katika taarifa, Sad Bouharrou, wa Kamati ya Misikiti ya Uholanzi-Morocco amesema, "vitendo visivyo na huruma kama yaliyojiri Quebec huchangua kuenea chuki dhidi ya Waislamu duniani."

Kwa msingi huo baada ya Waislamu kuingia ndani ya msikiti, wakati sala itakapoanza misikiti hiyo itafungwa ili kuzuia hujuma kama ile ya Quebec.

Amesema msikiti huwa wazi wakati wote wa siku kwa ajili ya watu wanaotaka kusali na kupata utulivu lakini amebainisha masikitiko yake kuwa wamelazimika kufunga misikiti wakati wa sala kutokana na kuhofua hujuma za kigaidi.

Uholanzi inajulikana kwa watu wenye chuki dhidi ya Uislamu hasa mwanasiasa Geert Wilders ambaye ni maarufu kwa misimamo yake mikali ya kibaguzi na chuki dhidi ya Waislamu.

Akizungumza mwezi Agosti mwaka jana, Wilders alisema kuwa, endapo chama chake kitashinda katika uchaguzi wa mwezi Machi, kitachukua maamuzi makali dhidi ya Waislamu.

Wilders alisisitiza kupitia taarifa ya kichochezi kuwa, kama atakuwa waziri mkuu wa Uholanzi, atapiga marufuku Qur'an tukufu na kufunga misikiti yote nchini humo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Wilders kutoa matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu. Kile kilichopelekea jina la Wilders kupata umashuhuri katika miaka ya hivi karibuni ni hatua yake ya kutengeneza filamu ya kuivunjia heshima Qur'an Tukufu ambacho ni kitabu cha mbinguni cha Waislamu, filamu iliyoitwa jina la 'Fitina.'

Utengenezwaji wa filamu hiyo uliibua malalamiko ya Waislamu duniani kote na hata kufunguliwa mashtaka dhidi ya mwanasiasa huyo katika mahkama za Uholanzi.

Kufuatia ushindi wa Donald Trump mwenye chuki dhidi ya Uislamu katika uchaguzi wa rais Marekani, wanasiasa wenye misimamo mikali ya mrengu wa kulia kote Ulaya nao pia wamepata matumaini ya kunyakua madaraka.

/3568706
captcha