iqna

IQNA

jcpoa
Uchambuzi wa kisiasa
TEHRAN (IQNA) - Kwa mujibu wa mtaalamu kutoka Ujerumani, mazungumzo kuhusu bei ya nishati na vile vile kutetea uhusiano wa kawaida kati ya Saudi Arabia na utawala wa Israel ni kati ya ajenda ya ziara ya kwanza ya Rais wa Marekani Joe Biden katika eneo la (Asia Magharibi) Mashariki ya Kati.
Habari ID: 3475468    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/06

Rais wa Iran katika mazungumzo na Rais wa Ufaransa
TEHRAN (IQNA)- Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mapatano yoyote yatakayofikiwa kwenye mazungumzo ya Vienna yenye lengo la kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA lazima yajumuishe suala la kuondolewa vikwazo taifa la Iran, sanjari na kupasishwa kwa kipengee kuhusu dhamana yenye itibari, na vile vile kujizuia na masuala ya kisiasa na kuibua tuhuma zisizo na msingi.
Habari ID: 3474953    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/20

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran amesisitiza kuwa msingi wa mazungumzo ya nyuklia JCPOA yanayofanyika mjini Vienna ni kuondolewa kwa mpigo vikwazo ilivyowekewa Iran.
Habari ID: 3474687    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/17

Rais wa Iran katika mazungumzo ya simu na Rais wa Ufaransa
TEHRAN (IQNA)- Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemfahamisha Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kuwa, Iran inataka kuona natija katika mazungumzo ya nyuklia yanayoendelea sasa Vienna Austria na kwamba lazima mazungumzo hayo yahitimishwe kwa Iran kuondolewa vikwazo.
Habari ID: 3474622    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/30

TEHRAN (IQNA) - Wabunge 200 wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) wametoa tamko la pamoja la kutaka kufutwa vikwazo vyote ilivyowekewa Iran.
Habari ID: 3473924    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/18

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumza kuhusu mapatano ya nyuklia ya JCPOA na vikwazo na kusema sera za Iran ziko wazi kuhusu JCPOA na vikwazo. Ameongeza kuwa sera hizo amezibainisha wazi kwa wakuu wa nchi kupitia maandishi na katika mikutano.
Habari ID: 3473814    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/14

Sheikh Naim Qassim
TEHRAN (IQNA)- Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, kuirejesha Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kutakuwa ni ushindi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3473804    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/12

TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, leo tunashuhudia mwanzo mpya wa kuhuishwa mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA.
Habari ID: 3473792    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/07

Rais Rouhani
TEHRAN (IQNA) -Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa, leo hii Marekani na serikali mpya ya nchi hiyo zimetambua kuwa zilifanya makosa kuhusu Iran na kueleza kuwa: Kusalimu amri mbele ya sheria si aibu na kwamba serikali ya Marekani haina budi ila kusalimu amri mbele ya sheria.
Habari ID: 3473662    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/18

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ameashiria hotuba yake ya hivi karibuni kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA baina ya Iran na nchi tano za kundi la 5+1 na kusema kuwa: Iwapo upande mwingine utatekeleza makubaliano hayo, Iran pia itatekeleza vipengee vyake, na mara hii Jamhuri ya Kiislamu haitatosheka kwa maneno na ahadi tupu.
Habari ID: 3473659    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/17

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Iran itarejea katika ahadi zake za makubaliano ya nyuklia ya JCPOA pale Marekani itakapoliondolea taifa hili vikwazo vyake vyote tena kivitendo na sio kwa maneno matupu au katika makaratasi tu.
Habari ID: 3473629    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/02/07

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametangaza bayana kuwa, kuingizwa Iran chanjo ya corona au COVID-19 kutoka Marekani na Uingereza ni marufuku.
Habari ID: 3473535    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/08

TEHRAN (IQNA) - Wabunge wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) wamelitaka Shirika la Atomiki la Iran kuzalisha urani iliyorutubishwa kwa zaidi ya asilimia 20 kwa ajili ya matumizi ya amani.
Habari ID: 3473412    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/01

TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi hii katu haitafanya mazungumzo kuhusu uwezo wa makombora yake ya kujihami.
Habari ID: 3473275    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/19

Rais Rouhani wa Iran
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Iran ameashiria pia kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Bahrain na utawala haramu wa Israel na kusema kuwa, watawala wa baadhi ya mataifa ya Kiarabu katika Asia Magharibi hawafungamani na malengo ya taifa madhulumu la Palestina.
Habari ID: 3473176    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/16

Rais Hassan Rouhani wa Iran
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema jitihada mpya za Marekani za kutumia azimio 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kutoa pigo kwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA tayari zimeshafeli.
Habari ID: 3473084    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/19

TEHRAN (IQNA)- Marekani imefedheheka duniani baada ya kushindwa katika jitihada zake za kulishawishi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa urefusha muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Habari ID: 3473069    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/15

Rais wa Iran katika mazungumzo ya simu na Rais wa Ufaransa
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na mwenzake wa ufaransa akisema kuwa Marekani daima imekuwa ikifanya jitihada za kuua mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusisitiza kuwa: Ulaya haipasi kukubali kuburutwa na Marekani na kutumbukia katika mtego wake.
Habari ID: 3473063    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/13

Rais wa Iran katika mazungumzo ya simu na Rais wa Russia
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na Rais Vladimir Putin wa Russia ameyahimiza mataifa ya dunia kusimama pamoja kukabiliana na ubabe wa Marekani wa kuchukua maamuzi ya upande mmoja.
Habari ID: 3472969    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/16

Kwa mnasaba wa kufikiwa mapatano ya JCPOA
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametuma ujumbe kwa mnasaba wa mwaka wa tano wa kufikiwa mapatano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) na kusema: "Kitendo cha Marekani cha kudhalilisha sheria na udiplomasia ni jambo linalohatarisha usalama wa nchi hiyo na dunia kwa ujumla mbali na kuchafua jina la Washington katika uga wa kimataifa."
Habari ID: 3472962    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/14