IQNA

Kwa mnasaba wa kufikiwa mapatano ya JCPOA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aikosoa Marekani kwa kuhatarisha usalama wa dunia

20:51 - July 14, 2020
Habari ID: 3472962
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametuma ujumbe kwa mnasaba wa mwaka wa tano wa kufikiwa mapatano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) na kusema: "Kitendo cha Marekani cha kudhalilisha sheria na udiplomasia ni jambo linalohatarisha usalama wa nchi hiyo na dunia kwa ujumla mbali na kuchafua jina la Washington katika uga wa kimataifa."

Katika ujumbe kupitia Twitter siku ya Jumanne, Zarif amesema mapatano ya JCPOA yalikuwa kati ya mafanikio makubwa ya muongo uliopita na kwa mara nyingine serikali ya Marekani inakosolewa kwa hatua zake zisizo za kisheria kuhusu mapatano hayo.

Zarif ameashiria kujiondoa kinyume cha sheria Marekani katika mapatano ya JCPOA na kusema: "Tabia ya Marekani ya kukwepa sheria haipaswi kuwa kigezo cha desturi za kimataifa."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika ujumbe wake huo wa Twitter amesema katika kipindi cha miaka mitano, Iran imefungamana na mapatano ya JCPOA ambayo yamekiukwa mara kadhaa na Marekani.  Aidha amesema Iran haijawahi kupokea himaya iliyoahidiwa na nchi za Magharibi zilizosalia katika JCPOA baada ya Marekani kujiondoa.

Aidha Zarif ameongeza kuwa, kwa matazamo wa Iran, udiplomasia una umuhimu na kwamba: "Jamuri ya Kiislamu ya Iran haitamruhusu mbabe adhoofishe maslahi ya Iran kwa kuitisha jamii ya kimataifa.

Baada ya miaka 13 ya mazungumzo magumu ya kimataifa, hatimaye tarehe 14 Julai mwaka 2015 kulifikiwa makubaliano ya nyuklia ya  Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).Mapatano hayo yalikuwa baina ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kundi la 5+1 ambalo lilijumuisha Russia, China, Marekani, Uingereza na Ufaransa pamoja na Ujerumani na halikadhalika Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya.

Marekani ilianza kukiuka mapatano hayo katika sku za awali za kuanza kutekelezwa kwake na baada ya Donald Trum kuchukua hatamu za uongozi Marekani, ukiukwaji huu ulishika kasi zaidi.

Hatimaye Mei 8 2018, Trump alichukua uamauzi wa upande mmoja wa kukiuka mapatano ya JCPOA. na kutakngaza kujiondoa katika mapatano hayo ya kimataifa. Baada ya hapo Trump alirejesha vikwazo vilivyo kinyume cha sheria dhidi ya Iran.

602758

Kishikizo: zarif ، iran ، JCPOA
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha