IQNA

Rais Rouhani wa Iran

Watawala wa baadhi ya nchi za Kiarabu hawafungamani na malengo ya Palestina

21:06 - September 16, 2020
Habari ID: 3473176
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Iran ameashiria pia kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Bahrain na utawala haramu wa Israel na kusema kuwa, watawala wa baadhi ya mataifa ya Kiarabu katika Asia Magharibi hawafungamani na malengo ya taifa madhulumu la Palestina.

Rais Rouhani amesema hayo leo katika kikao na baraza  la mawaziri ambapo ameonya kuwa, matokeo yote mabaya ya kuanzisha uhusiano na Israel yatakuwa katika dhima na mabega ya mataifa ambayo yameanzisha uhusiano na Wazayuni kinyume kabisa na kanuni na usalama wa eneo hili.

Kwingineko, Rais Rouhani amesema   kuwa, Marekani imefeli na kushindwa katika juhudi zake za kutaka kutumia utaratibu wa kusuluhisha mzozano katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, unaojulikana kama 'Utaratibu wa Kifyatuo' kwa kimombo "Trigger Mechanism".

ameashiria juhudi za Marekani za kutaka kutumia 'Utaratibu wa Kifyatuo' na kusema kuwa, utaratibu huo ni kwa ajili ya nchi wanachama wa makubaliano ya JCPOA.

Rais wa Iran amesema kuwa, taifa ambalo liliyataja makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kuwa ni mapatano mabaya zaidi katika historia ya Marekani na likajitoa katika makubaliano hayo ya kimataifa, halina haki ya kuzungumzia na kutoa maoni kuhusiana na 'Utaratibu wa Kifyatuo'.

Dakta Hassan Rouhani amesema kuwa, Marekani inataka kuanzisha njama mpya dhidi ya Jamhuri ya Kiisamu ya Iran na kuongeza kuwa, wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na mataifa matatu ya Ulaya yamebainisha wazi kwamba, yanapinga kutumiwa utaratibu huo.

3923309

captcha