IQNA

Rais wa Iran katika mazungumzo ya simu na Rais wa Russia

Kuna udharura wa kukabiliana na ubabe wa Marekani

17:22 - July 16, 2020
Habari ID: 3472969
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na Rais Vladimir Putin wa Russia ameyahimiza mataifa ya dunia kusimama pamoja kukabiliana na ubabe wa Marekani wa kuchukua maamuzi ya upande mmoja.

Mazungumzo hayo ya simu yamefanyika leo Alkhamisi na pande mbili zimejadiliana njia za kustawisha ushirikiano baina yao katika nyuga zote za kisiasa, kiuchumi, kielimu na kiutamaduni. Aidha Rais Rouhani ameelezea kufurahishwa kwake na jinsi mazungumzo ya viongozi wa nchi hizi mbili yanayovyotekelezwa kivitendo.

Pia ameashiria mazungumzo ya marais wa nchi tatu za Iran, Russia na Uturuki yaliyofanyika kwa njia ya video kwa shabaha ya kuleta utulivu, amani na usalama nchini Syria na kuhimiza kuendelea ushirikiano wa nchi hizo tatu kupitia mazungumzo ya Astana kwa ajili ya kulifanikisha jambo hilo hususan misaada ya kibinadamu.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametilia mkazo pia wajibu wa kutekelezwa kikamilifu mapatano ya nyuklia ya maarifi kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA ) ambayo ni makubaliano ya kimataifa yenye baraka kamili za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuyataka mataifa ya dunia kuungana katika kukabiliana na ubeberu wa Marekani na kukomeshwa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran.

Rais Rouhani pia ameishukuru Russia kwa uungaji mkono wake kwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA,

Kwa upande wake Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa nchi yake inaendelea kuunga mkono kikamilifu makubaliano ya JCPOA kama ilivyofanya kwa muda wa miaka mitano sasa ya kufikiwa mapatano hayo na amesema ni jambo la dharura kulindwa na kuhifadhiwa makubaliano hayo ya kimataifa. Pia amesema nchi yake itaendelea kuunga mkono misimamo ya Iran katika jamii ya kimataifa.

3910903

Kishikizo: Iran ، Putin ، Rouhani ، JCPOA
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha