IQNA

Mashia wa Bahrain hawapewi kazi idara za serikali

9:11 - November 03, 2013
Habari ID: 1309363
Katibu Mkuu wa chama cha al Wifaq cha Bahrain amesema kuwa Waislamu wa madhehebu ya Shia na wapinzani wa utawala wa kizazi cha Aal Khalifa wananyimwa kazi katika idara za serikali ya Manama kwa sababu za kimadhehebu na kisiasa.

Sheikh Ali Salman amesema kuwa Wabahrain elfu nne wamenyimwa ajira katika ofisi na idara za serikali kwa sababu za kimadhehebu na kisiasa.

Sheikh Salman amongeza kuwa, badala yake watawala wa Manama wanawaajiri madaktari, wauguzi, walimu na wafanyakazi wa kigeni na hata wanawapa uraia wa Bahrain baadhi yao.

Jumuiya za kimataifa za kutetea haki za binadamu zinailaumu sana serikali ya Bahrain kwa kuwakandamiza Waislamu waliowengi wa madhehebu ya Shia nchini humo na kuwanyima haki zao za kimsingi. 1310163   

captcha