Kitengo cha Shughuli za Wanawake, kilicho chini ya Kituo cha Elimu ya Qur’ani cha Idara ya Mfawidhi (Astan) ya Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS), ndicho kilichoandaa mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yalianza Jumatatu, Agosti 10, baada ya kukamilishwa kwa maandalizi yote ya awali yaliyohitajika. Wissam Nazir Al-Dulfi, mkuu wa Kituo cha Habari cha Qur’ani cha idara hiyo, amesema mafunzo hayo yanaendeshwa kwa ushiriki wa waalimu 100 wa kike wa Qur’ani kutoka katika kituo hicho.
Ameeleza kuwa programu hiyo inajumuisha masomo ya Qur’ani, dini, fiqhi na itikadi, pamoja na masomo ya tafsiri ya Qur’ani kwa kuzingatia mada mbalimbali. Al-Dulfi ameongeza kuwa wasimamizi 50 watasimamia upangaji na uelekezaji wa wanafunzi wa Qur’ani katika maeneo mbalimbali ya Haram Tukufu, huku mabasi 50 yakitengwa kwa ajili ya usafiri wao. Kwa mujibu wa Al-Dulfi, jumla ya wasichana 2,500 watakubaliwa kushiriki katika mafunzo hayo.
Washiriki hao wanatoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Karbala, wakiwemo raia wa nchi za Kiarabu na za kigeni wanaoishi katika mkoa huo, na wanatoka katika makundi mbalimbali ya umri. Lengo ni kuwawezesha washiriki wote kujifunza elimu ya Qur’ani na kueneza utamaduni wake usio na mipaka.
Inafaa kutajwa kuwa wafanyakazi wa utawala, mahusiano ya umma na huduma wamekamilisha maandalizi yote muhimu kwa ajili ya kutekeleza mpango huu, pamoja na kufanya uratibu unaohitajika na idara mbalimbali za usaidizi za Astan.
3498630