IQNA – Harakati ya Muqawama wa Palestina ya Hamas imepongeza kauli ya Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, kuhusu umuhimu wa kusitishwa kwa vita katika ukanda wa Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).
Basem Naim, mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas, amesema harakati hiyo inathamini sana kauli za Rezaei kuhusu ulazima wa kusitisha vita katika ukanda mzima, hususan nchini Lebanon na Ukanda wa Gaza.
Katika ujumbe aliouchapisha kwenye jukwaa la X siku ya Alhamisi, Naim amesema: “Kusitisha vita hivi ni maslahi ya juu kabisa kwa ukanda huu, wananchi wake na mustakabali wake.”
Amesisitiza kwamba “kuendelea kwa vita hivi kunawanufaisha tu maadui wa Kizayuni katika mipango yao ovu dhidi ya Umma wetu, mipango inayolenga kuusambaratisha ukanda huu, kuuvuruga na kupora rasilimali zake.”
Awali, Rezaei alisisitiza katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba Marekani inapaswa kusitisha uchokozi wake dhidi ya Iran, kuachilia mali za Iran zilizogandishwa, na kukomesha vita vinavyoendelea katika ukanda huu, hususan nchini Lebanon na katika Ukanda wa Gaza.
3498634