IQNA-Haram takatifu ya Imam Ali (AS) mjini Najaf, Iraq, imepokea zaidi ya vikundi 100 vya maombolezo na wajumbe mbalimbali katika usiku wa kuamkia tarehe 28 Safar.
Hassan Zaki, mmoja wa watumishi wa Haram ya Imam Ali (AS), ameeleza kuwa kwa uratibu wa idara husika za usaidizi, harakati za vikundi hivyo zaidi ya 100 zilirahisishwa. Kati ya vikundi hivyo, minane mikubwa ilifanya ibada za maombolezo ndani ya uwanja wa Haram, huku vikundi vingine vikiingia na kufanya ibada zao katika maeneo ya pembezoni ya mji huo mtukufu.
Ali Abdul Zaid Kazim, mtumishi mwingine wa Haram ya Alawi, amebainisha kuwa uongozi wa Haram hiyo takatifu umetumia nguvu zake zote kutoa huduma bora zaidi kwa Mazuwar wanaozuru kaburi hilo tukufu.
Huduma hizi zinajumuisha ugawaji wa milo mitatu kwa siku, pamoja na kutoa mahali pa kupumzika na malazi, yote hayo yakiwa na lengo la kuhakikisha ustawi na faraja ya Mazuwar katika kipindi hiki cha hija ya maombolezo.
Kazim alibainisha kuwa shughuli hizi za kuhudumia Mazuwar zilianza tarehe 10 Safar na zitaendelea hadi mwisho wa maadhimisho ya kumbukumbu ya kufariki kwa Mtume Muhammad (SAW).
Tarehe 28 ya mwezi wa Safar—mwezi wa pili katika kalenda ya Hijria, ambayo mwaka huu imeangukia siku ya Jumatano, Agosti 12, ni siku ya maombolezo makubwa ya kuadhimisha kufariki kwa Mtume Muhammad (SAW) pamoja na shahada ya Imam Hassan (AS), Imam wa pili wa Kishia.
3498623