IQNA

Ikhwanul Muslimin yaitisha mazungumzo Misri

11:38 - November 17, 2013
Habari ID: 1318451
Harakati ya Ikhwanul Muslimin nchini Misri imetoa wito wa kufanyika mazungumzo ili kumaliza mgogoro wa kisiasa ulioibuka nchini humo baada ya rais Mohammad Mursi kuondolewa madarakani mwezi Julai.

Hayo yamebainika katika taarifa iliyotolewa Jumamosi na Muungano wa Kitaifa wa Kuunga Mkono wa Kisheria ambao unaongozwa na Harakati ya Ikhanul Muslimin. Muungano huo umekuwa ukiandaa maandamano tokea Mursi alipopinduliwa. Katika taarifa, muungano huo umetoa wito kwa  vyama vya kisiasa na wazalendo kuanzisha mazungumzo ya kina ili kutafuta njia za kuiondoa nchi hiyo katika mgogoro na kuhitimisha utawala wa kijeshi.


Misri ilitumbukia katika ghasia na machafuko tokea Julai 3 mwaka huu wakati jeshi lilipompindua rais Mursi na kumteua jaji wa Mahakama ya Katiba Adly Mahmoud Mansour kukaimu nafasi ya rais. Zaidi ya wafuasi 2,000 wa Mursi wameuawa katika kipindi cha miezi mitano iliyopita kufuatia hujuma ya vikosi vya usalama dhidi ya wanaopinga mapinduzi ya kijeshi.


1318246
captcha