IQNA

Kiongozi Muadhamu amuomboleza mwanazuoni wa Masunni Iran

22:19 - April 26, 2014
Habari ID: 1399942
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa salamu za rambi rambi kufuatia kifo cha mjumbe wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi na Imam wa Sala ya Ijumaa wa Jamii ya Masunni katika mji Sanandaj magharibi mwa Iran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Katika ujumbe wake, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemtaja marehemu Mamusta Hissamuddin Mojtahidi kuwa shakhsia mwenye kujitolea kuhudumu ambaye aliwasomesha wanazuoni wengi katika eneo. Aidha amemtaja mwanazuoni huyo aliyeaga dunia kuwa aliyekuwa mtiifu kwa ujumbe wa kimapinduzi wa umoja wa Waislamu na kwamba alijitahidi kuleta ukuruba baina ya madhehebu ya Kiislamu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewapa mkono wa pole watu wote waumini na wanamapinduzi wa eneo la Kurdistan pamoja na familia na jamaa kufuatia kuaga dunia mwanazuoni huyo maarufu wa madhehebu ya Shafi.
Naye Rais Hassan Rouhani wa Jmahuri ya Kiislamu ya Iran pia ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kuaga dunia Mamusta Hissamuddin. Amesema katika umri wake uliojaa baraka, mwanzuoni na imamu huyo wa Ahli Sunna katika eneo la Kurdistan alijitahidi kuleta umoja wa Kiislamu.

1399937

captcha