IQNA

Nakala milioni moja za Qur'ani zagawiwa Masjidul Haram

16:28 - July 06, 2014
Habari ID: 1426540
Idara inayosimamia masuala ya Msikiti Mtakatifu wa Makka na Msikiti wa Mtume (saw) mjini Madina imegawa nakala milioni moja za tarjumi za Qur'ani kwa lugha 41 katika Masjidul Haram kwa mnasaba wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Mkurugenzi wa Idara ya Qur'ani na Vitabu vya Msikiti wa Makka amesema kuwa idara inayosimamia msikiti huo na ule wa Mtume mjini Madina inafanya jitihada za kudhamini nakala za Qur'ani zinazohitajika katika Msikiti wa Makka. Sheikh Muhammad al Silani amesema kuwa nakala 144 za tarjumi hizo za Qur'ani zimeandikwa kwa hati za blail.
Sheikh Silani ameongeza kuwa mpango maalumu wa mwezi Ramadhani wa kugawa nakala milioni moja za Qur'ani unajumuisha ukusanyaji wa nakala za zamani, kuitisha vikao vya kusahihisha qiraa na kuchapisha vitabu vya kulingania dini na kuvisambaza.
Sheikh Al Silani amewataka watu waliokwenda kuzuru maeneo matakatifu wasitumie mikoba makhsusi ya nakala za Qur'ani kwa ajili ya vitu vingine visivyokuwa Qur'ani.

1426271

captcha