IQNA

Umrah

Zaidi ya waumini milioni 10 wametembelea Al-Rawdah Al-Sharif hadi sasa mwaka 2024

18:38 - October 14, 2024
Habari ID: 3479591
IQNA - Zaidi ya waumini milioni 10 wameswali katika Al-Rawdah Al-Sharif kwenye Msikiti wa Mtume (Al-Masjid an-Nabawi) kuanzia mwanzoni mwa 2024.

Takwimu hizo, zilizotolewa na Mamlaka ya Utunzaji wa Masuala ya Msikiti wa Mtume, zinaonyesha kuwa wanaume 5,583,885 na wanawake 4,726,247 wameswali katika Al-Rawdah Al-Sharif mwaka huu.

Msikiti wa Mtume (Al-Masjid an-Nabawi) ulioko Madina, Saudi Arabia ni eneo iliko Al-Rawda Al-Sharifa ambapo kaburi la Mtume Muhammad (SAW) lipo.

Takwimu pia zilionyesha kuwa wastani wa muda wa kusubiri kabla ya kuingia Al-Rawdah Al-Sharif ulikuwa dakika 20, na idadi ya wageni kwa siku ilifikia hadi 48,000.

3490276

Habari zinazohusiana
captcha