Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA Afrika Mashariki, hafidh na qarii kutoka Iran pamoja na kundi la Qasida walishiriki katika hafla ambayo ilifanyika Kampala, mji mkuu wa Uganda na kuhudhuria pia na Musa Ali Naibu Waziri Mkuu wa Uganda, Naibu Waziri wa Afya, wabunge, mabalozi na wawakilishi wa nchi za Kiislamu kama vile Sudan, Saudi Arabia, Imarati, Libya na Misri.
Aidha hafla hiyo ilihudhuriwa pia na wahadhiri wa vyuo vikuu, mwakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt AS, mwakilishi wa Chuo Kikuu cha AL Mustafa AS Bw. Amir Hussein Nikbein, Balozi wa Iran nchini Uganda na Mwambata wa Utamaduni wa Iran katika jengo la Ubalozi wa Iran mjini Kampala.