Ayatullah Araki amesisitiza kuwa, miongoni mwa majukumu muhimu ya mfumo wa Kiislamu ni kuleta umoja na mshikamano baina ya Waislamu. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuzikurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu ameongeza kuwa, umoja ni msingi wa nguvu kwa jamii za Kiislamu. Ayatullah Muhsin Araki amebainisha kwamba, maadui wa Uislamu wanaulenga umoja wa jamii ya Kiislamu na wanafahamu kwamba, nguvu ya Waislamu iko katika umoja wao. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kuzikurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu ameeleza kuwa, ni kwa kuzingatia ukweli huo ndio maana maadui wamekuwa wakifanya njama za kuusambaratisha umma wa Kiislamu sambamba na kupanda mbegu za chuki na hasama baina ya makundi, madhehebu na kaumu mbalimbali katika ulimwengu wa Kiislamu.