Akizungumza na IQNA, Sheikh Farajullah Shazli amesema mashindano hayo ambayo huwaleta pamoja wanafunzi Waislamu kutoka vyuo vikuu kote duniani ni njia muafaka ya kutumia Qur'ani katika kuleta mashikamano baina ya Waislamu .
Amependekeza kuwa mbali na mashindano ya qiraa na hifdh ya Qur'ani Tukufu, kunapaswa pia kuanzishwa kategoria zingine kama vile tafsiri ya Qur'ani katika mashindano hayo.
Sheikh Shazli ambaye amewahi kuwa katika jopo la majaji katika mashindano yaliyotangulia ya Qur'ani ya wanachuo amepongeza kiwango kizuri cha mashindano hayo. Halikadhalika ametoa wito wa kujumuishwa wanafunzi wa kike katika mashindano hayo ili kustawisha utamaduni wa Qur'ani miongoni mwa wanawake.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu hufanyika kila miaka miwili nchini Iran chini ya usimamizi wa Taasisi ya Kiakademia ya Harakati za Qur'ani Iran. Hadi sasa mashindano hayo yameshafanyika katika miji ya Iran ya Isfahan, Tehran, Mashhad na Tabri. Duru ya tano ya mashindano hayo inatazamiwa kufanyika mwaka ujao wa 2015.
1441962