IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Wanachuo walioshinda Mashindano ya Qur’ani ya Taifa watunukiwa zawadi

21:40 - September 12, 2024
Habari ID: 3479421
IQNA - Sherehe ya kutunuku washindi wa toleo la 38 la Mashindano ya Qur’ani na Etrat ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Iran ilifanyika Tabriz siku ya Jumatano.

Maafisa kadhaa akiwemo Mkuu wa Ofisi ya Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Vyuo Vikuu Hujjatul Islam Rostami, walihudhuria hafla hiyo.

Washindi wa kategoria tofauti walitambulishwa na kutunukiwa zawadi katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Tabriz cha Sayansi ya Tiba.

Jumla ya washindani 277 walishindania tuzo ya juu katika kategoria tofauti katika sehemu za wanaume na wanawake.

Walikuwa wametinga fainali baada ya kuonyesha utendaji bora katika raundi za awali.

Tarteel, usomaji wa Qur'ani, kuhifadhi Qur'ani katika viwango tofauti, usomaji wa du'a na usomaji wa mashairi ya kidini ni miongoni mwa kategoria za mashindano ya mwaka huu.

Jumla ya wataalamu 45 wa Qur'ani walihudumu katika majopo ya majaji katika sehemu za wanaume na wanawake.

Hafla hiyo ya kila mwaka huandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Sayansi, Utafiti na Teknolojia na Wizara ya Afya na Sayansi ya Tiba.

Inalenga kukuza mafundisho ya Qur'ani miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

4236113

Habari zinazohusiana
captcha