IQNA

Azma yetu ni kutokomeza magaidi wote

20:19 - October 14, 2014
Habari ID: 1460245
Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, harakati hiyo imeazimia kupambana na makundi ya kitakfiri na magaidi licha ya mashinikizo yanayoikabili nchi hiyo hivi sasa.

Sayyid Nasrullah ameyasema hayo leo wakati alipotembelea eneo la Biqaa. Katibu Mkuu wa Hizbullah ametoa wito wa kusafishwa kikamilifu eneo la Qalamun na kurejeshwa mawasiliano na maeneo mengine ikiwemo al-Zabadani ambayo yanakabiliwa na hali mbaya baada ya magaidi wa Daesh kushadidisha mashambulizi yao katika barabara kuu ya Qalamun. Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kuwa, mapambano yanayomtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu hayatakiwi kurudi nyumana kwamba kujitolea kwa mashahidi na majeruhi wanaolitakia kheri taifa la Lebanon, kutazaa matunda makubwa. Akiashiria operesheni iliyofanywa na Hizbullah dhidi ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika eneo la Shaba'a wiki moja iliyopita, Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, operesheni hiyo ilikuwa na ujumbe muhimu kwamba, licha ya mabadiliko yanayojiri sasa na uvamizi wa majeshi ya muungano wa kimataifa kwa kile kinachosemwa kuwa ni mashambulizi dhidi ya kundi la Daesh, muqawama bado una uwezo mkubwa wa kukabiliana na adui.  AIR 1460026

captcha