Jaji huyo amesema kuwa marufuku hiyo haikiuki haki za kiraia za wanafunzi. Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu ya Nigeria iliwasilisha kesi hiyo mahakamani ikihoji marufuku hiyo dhidi ya hijabu katika shule za msingi na upili, ambayo ilitangazwa katika mji wa Lagos mwaka uliopita. Akijibu kesi hiyo,Jaji Mdopue Onyeabo wa Mahakama Kuu ya Lagos alisema hapo jana kuwa marufuku hiyo dhidi ya vazi la Kiislamu la Hijabu kwa shule za serikali katika mji wa Lagos, haikiuki haki za kimsingi kwa dini za wananafunzi hayo, kwa kuwa Nigeria ni nchi ya Kiseikulari ambayo haihesabu dini yoyote kama dini ya nchi.
Wakati huo huo weledi wa mambo wameitaja hatua hiyo ya Mahakama Kuu ya Lagos kuwa ina malengo maalumu na inakinzana na uhuru wa kiraia. Sheria inayopiga marufu vazi la hijabu katika shule za serikali katika mji wa Lagos ilipasishwa mwaka mwaka 2013. Hata hivyo malalamiko yaliyowasilishwa na Taasisi ya Wanafunzi wa Kiislamu ya Nigeria ikipinga sheria hiyo ilipelekea kuakhirishwa utekelezwa wake. Wanachama karibu 200 wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kike Waislamu walikusanyika mkabala na jengo la Mahakama Kuu ya Nigeria kupinga sheria hiyo. Wakili wa utetezi wa jumuiya hiyo ya wanafunzi Waislamu wa Nigeria pia amewasilisha ombi akitaka kuangaliwa upya sheria hiyo inayopiga marufuku vazi la hijabu katika shule za serikali katika mji wa Lagos.
Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, kuidhinishwa sheria hiyo inayozuia vazi la stara la mwanamke wa Kiislamu hijabu katika shule za serikali, hususan katika kipindi cha sasa ni kitendo kisicho cha busara na cha uchochezi. Hivi karibubu jeshi la Nigeria lilitangaza kuwa limefanya mazungumzo na viongozi wa kundi la Boko Haram katika jitihada za kuwaachia huru wanafunzi wa kike wanaoshikiliwa na kundi hilo na kwa ajili ya kusitisha mapigano. Hata hivyo hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu namna usitishaji mapigano kati ya pande mbili hizo utakavyotekelezwa na jindi mabinti hao watakavyokabidhiwa kwa viongozi wa serikali.
Wanachama wa kundi la Boko Haram mwanzoni mwa mwaka huu walishambulia bweni la wanafunzi wa kike katika eneo la Chibok nchini Nigeria na kuwateka nyara wanafunzi zaidi ya 270. Baadhi ya wanafunzi hao walifanikiwa kutoroka. Kabla ya hapo wanamgambo wa kundi la Boko Haram walitangaza kuwa watawauza wasichana hao kwa waasi wa Chad.
Baadhi ya wataalamu wanaamini kuwa hatua ya sasa ya mahakama ya Nigeria ni ushahidi mwingine wa misimamo isiyo sahihi ya Rais Goodluck Jonathan. Wataalamu hao wanasema kuwa serikali kibaraka ya Jonathan ambayo ilichukua madaraka ya nchi kwa uungaji mkono wa siri wa Marekani, inalenga kuchafua sura ya Uislamu na Waislamu. Wataalamu hao wanathubutu hata kusema kuwa serikali ya sasa ya Abuja inawaunga mkono na kufanya kazi na wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram kwa lengo la kuwafanya watu wauchukie Uislamu na kuwachafulia jina Waislamu wa Nigeria.../mh