IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani yaanza Makka

16:53 - November 15, 2014
Habari ID: 1473482
Duru ya 36 ya Mashindano ya Kimatiafa ya Hifdhi, Qiraa na Tafsiri ya Qur’ani Tukufu yameanza leo Novemba 15 katika Msikitu Mkuu wa Makka (Masjid al-Haram) , Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa gazeti la Okaz, mashindano hayo yameandaliwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu na Awqaf nchini Saudi Arabia.
Mashindano hayo yatafanyika ndani ya kumbi kadhaa za Masjid al-Haram hadi tarehe 19 Novemba.
Vitengo vya mashindano hayo vitajumuisha kuhifadhi Qur’ani kikamilifu na kuisoma kwa tajweed, kuhifadhi Qur’ani kikamilifu na kuisoma kwa tajweed pamoja na tafsiri yake, kuhifadhi juzuu 15 na kuhifadhi juzuu 5.
Washiriki kutoka nchi zisizo za Kiislamu ndio pekee watakaoruhusiiwa kushiriki katika mashindano ya kuhifadhi Juzuu 5.
Mashindano ya mwaka huu yana washiriki 138 kutoka nchi 59.../mh

1473128

captcha