IQNA

Makanisa yazidi kufungwa nchini Ujerumani

12:04 - November 05, 2008
Habari ID: 1704824
Idadi ya Makanisa yanayofungwa kutokana na kuongezeka kodi na kukosa uwezo wa kulipa ada za serikali inazidi kuongeza nchini Ujerumani.
Mwandishi wa kujitolea wa IQNA amesema kuwa, kwa sasa kanisa moja kati ya kila makanisa manne ya Ujerumani linakabiliwa na hatari ya kufungwa. Amesema kuwa, baadhi ya makanisa ya Ujerumani yanalazimika kutekeleza ada zao za kidini katika mahema.
Askofu wa eneo la Essen huko Ujerumani amesema kuwa, shughuli kubwa za kidini zitasimamishwa baada ya makanisa kuhamishiwa katika mahema ya plastiki na kwamba makasisi hawatakuwa na kazi nyingine ghairi ya kutoa mawaidha kwa watu. 315657


captcha