Kama serikali za nchi za Kiislamu zingechukua hatua ya kubuni soko na baraza la kimataifa la Waislamu katika msimu wa hija na katika mazingira ya amani na utulivu yanayotawala katika msimu huu, ambapo umati mkubwa wa Waislamu huwa wamekusanyika sehemu moja na kwa wakati mmoja, umma wa Kiislamu haungeonekana kuwa dhaifu mbele ya madola makubwa yenye kiburi duniani
Hayo yamesemwa na Hujjatul Islam wal Muslimeen Sayyid Fadhli Askar, Nauu Mkuu wa taasisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran inayoshughulikia masuala ya mahujaji. Huku akibainisha athari muhimu za hija katika kubadilisha na kurekebisha tabia za kijamii na kimaadili za Waislamu, Sayyid Askar amesema kuwa mjumuiko mkubwa wa Waislamu katika hija ambao huwapa nafasi ya kukutana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yanayotokea duniani, huwawezesha pia kuwa na nafasi muhimu katika mkondo wa matukio ya dunia. Akizungumzia umuhimu wa Waislamu kukutana sehemu moja kwa ajili ya kuzungumzia masuala na matatizo yanayowakabili, Sayyid Askar amesisitiza kwamba, hata kabla ya mwanadamu kufikiria umuhimu wa kubuni jumuiya kama vile za Umoja wa Mataifa, Mwenyezi Mungu tayari alikuwa amewaandalia wanadamu sehemu ya kukutana na kukusanyika kwa lengo la kujadili masuala na changamoto mbalimbali zinazowakabili maishani, kwa kuwaandalia sehemu tulivu ya mijumuiko kama hiyo huko katika ardhi ya Makka, Saudi Arabia. Akiashiria utulivu na amani inayotawala katika eneo hilo tukufu, Hujjatul Islam Fadhli Askar amesisitiza kwamba, amani hiyo haihusiani na wanadamu peke yao bali, bali hata wadudu na mimea ambayo haipasi kudhuriwa na mwanadamu katika sehemu hiyo takatifu. Amegusia masaibu na mikasa inayowapa Waislamu katika ulimwengu wa Kiislamu na hasa katika nchi za Iraq, Pakistan, Palestina na Afghanistan kutokana na siasa mbovu za madola makubwa na kusema kuwa inasikitisha kuona kwamba katika mazingira kama hayo kuna baadhi ya viongozi wa nchi za Kiislamu wanaokutana na Wazayuni na waungaji mkono wao wa Magharibi kwa lengo la kujadili masuala yasiyo na natija yoyote isipokuwa madhara kwa ulimwengu wa Kiislamu.316803