Kwa mujibu wa Al-Kafeel, Astan imeanzisha mawakib za kiutamaduni katika njia kuu tatu zinazoelekea katika mji mtakatifu wa Karbala, ambazo ni njia za Baghdad, Najaf na Babylon. Mawakib hizo zimeanzishwa kwa ushirikiano wa idara mbalimbali za Astan, kwa lengo la kutoa programu za kidini, kiutamaduni, kiakili, kielimu na za kuimarisha uelewa kwa mazuwar wa Arbaeen.
Mawkib (kwa wingi Mawakib) kimsingi ni mahema au vituo vinavyowekwa kando ya barabara zinazoelekea mji mtukufu wa Karbala na ndani ya mji huo wenyewe, kwa ajili ya kutoa huduma za chakula cha nadhiri, vinywaji, malazi, na huduma nyinginezo bila malipo kwa mazuwari wa Arbaeen.
Sayyed Ahmad Sadiq, anayesimamia Mawkib ya Kiutamaduni iliyoko kwenye njia ya Najaf, alisema kituo hicho kinawapokea kila siku maelfu ya mazuwar kutoka nchi mbalimbali wanaoshiriki katika matembezi au Mashaya ya Arbaeen. Alibainisha kuwa njia ya Najaf–Karbala ni miongoni mwa njia muhimu zaidi na zenye msongamano mkubwa wa mazuwar wanaoelekea katika mji mtakatifu wa Karbala.
Alisema Mawkib hiyo inaendelea kuendesha programu zake za kiutamaduni, kidini na kielimu, ambazo zina mchango mkubwa katika kuinua kiwango cha uelewa wa kidini na kiutamaduni miongoni mwa mazuwar. Kwa mujibu wa Sadiq, shughuli za Mawkib hiyo zinajumuisha kuandaa mashindano ya kiutamaduni, kutekeleza programu za uongofu wa kidini, kuandaa maonyesho ya vitabu na machapisho, pamoja na kuendesha mfululizo wa programu na shughuli shirikishi kwa ajili ya mazuwar.
3498492