Abdul Malik Dawoud, mkuu wa kamati inayoandaa mashindano hayo amesema kuwa maandamano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Wanazuoni Wanaohudumia Qur'ani na Sunna za Mtume Mtukufu (SAW), mashindano ambayo yanawashirikisha wahifadhi Qur'ani wapatao 128. Washindani wanaoshiriki katika mashindano hayo wamegawanywa katika makundi mawili ya wanaume na wanawake. Ameongeza kwamba katika duru hii ya tisa wahifadhi Qur'ani watashindana katika makundi matatu ya waliohifadhi juzuu 10 tu, waliohifadhi juzuu 20 na waliohifadhi Qur'ani nzima. Amesema, wawakilishi wa miko 15 na taasisi 28 za Qur'ani zinazofungamana na Wizara ya Elimu na Masomo ya nchi hiyo wanashiriki katika mashindano hayo. Daoud amesema kuwa lengo kuu la kuandaliwa mashindano hayo ni kuwashajiisha vijana wazingatie kitabu hicho kitakatifu, kunyanyua kiwango cha elimu cha wanafunzi na wanachuo na vilevile kuratibu shughuli za taasisi zinazojishughulisha na masuala ya Qur'ani kote nchini Yemen. Mwishoni Daoud amesema kuwa mashindano hayo yatakayoendelea kwa muda wa wiki moja yanawashirikisha wanawake kwa mara ya kwanza. 316991