IQNA

Jumuiya ya Kiislamu na Kikristo ya Kutetea Quds kuasisiwa

14:56 - November 10, 2008
Habari ID: 1706714
Jumuiya ya Kiislamu na kikristo ya kutetea Quds Tukufu ambayo lengo lake litakuwa ni kulinda athari za kihistoria za Quds Tukufu na kuimarisha uhusiano wa Waislamu na Wakristo katika uwanja huo inatarajiwa kuasisiwa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Palestina WAFA, lengo la jumuiya hiyo ni kuratibu na kuwasiliana na taasisi na jumuiya mbalimbali za Kiarabu na kimataifa kuhusu kadhia ya kulinda matukufu ya Kiislamu na Kikristo katika mji wa Quds na kuwapasha walimwengu habari na ripoti zinazohusiana na matukio yamji huo na njama za uharibifu za Wazayuni.
Malengo mengine ya jumuiya hiyo ni kushiriki katika harakati za kimataifa zinazohusiana na ukarabati wa Quds na kuratibu shughuli rasmi za wananchi katika medani hiyo.
Jumuiya hiyo itafanya kazi zake chini ya sheria za Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) na baraza la viongozi wake, ambalo litajumuisha shakhsia wa Kiislamu na Kikristo, litakuwa likichaguliwa kila baada ya kipindi cha miaka minne. 317708
captcha