IQNA

Dunia ya leo inahitajia dini na maadili.

10:29 - November 11, 2008
Habari ID: 1706935
Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kiislamu wa Misri Mahmoud Hamdi Zaqzouq amesema kuwa dunia ya leo inahitajia mafundisho ya dini na maadili mema.
Hamdi Zaqzouq ameyasema hayo katika kongamano la Mazungumzo ya Uislamu na Ukristo” lililofanyika jana nchini Ujerumani.
Waziri wa Waqfu wa Misri amesema dini za mbinguni za Uislamu na Ukristo zina vigezo na misingi mingi inayofanana na kwamba wasomi wa Kiislamu na Kikristo wanaweza kutumi misingi hiyo kwa ajili ya kutafuta njia za ufumbuzi wa mtatizo ya dunia ya sasa.
Zaqzouq amesema, mazungumzo kati ya wafuasi wa dini mbalimbali katika zama hizi za utandawazi ni jambo la dharura ambalo haliwezi kufumbiwa macho na Waislamu na Wakristo.
Waziri wa Waqfu wa Misri amesema kuwa siasa za kupuuza na kutotambuana haziwezi kukubalika na kwamba mgogoro wa fedha ulioikumba dunia umeonyesha kwamba nchi zote zinathirika na matatizo ya zama hizi. Ameongeza kuwa mafanikio ya mazungumzo kati ya dini na tamaduni mbalimbali yanahitaji kutambuana na kuheshimiana, suala ambalo hujenga hali ya kuaminiana na kuimarisha amani kote duniani.
Kongamano la mazungumzo ya Uislamu na Ukristo lililofanyika mjini Berlin, Ujerumani limehudhuriwa na wasomi wa Kiislamu na Kikristo. 318266
captcha