IQNA

Taasisi ya Quran ya haram ya Imam Hussein AS yafunguliwa

10:38 - November 11, 2008
Habari ID: 1706943
Kituo cha kuhifadhi Qur’ani cha haram tukufu ya Imamu Hussein bin Ali AS kimefunguliwa katika sherehe zilizohudhuriwa na shakhsia wa kidini na kitamaduni wa Iraq katika mji mtakatifu wa Karbala.
Mkurugenzi wa kituo hicho Hassan al Mansuri amesema lengo la kuasisiwa kituo cha kuhifadhi Qur’ani cha haram ya Imam Hussein AS ni kuwahamasisha watoto na vijana kusoma, kuhifadhi na kufasiri Qur’ani Tukufu. Al Mansuri amesema, malengo mengine ni kueneza utamaduni wa kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu katika matabaka mbalimbali ya jamii ya Iraq na kulea kizazi chenye maarifa ya Qur’ani Tukufu.
Mkurugenzi wa Kituo cha Qur’ani cha haramu ya Imam Hussein AS amevitaka vyombo vya habari hususan kanali za televisheni za satalaiti kurusha hewani vipindi vinavyowahimiza watu kuipenda Quran na Ahlubaiti wa Mtume Muhammad SAW na kuwafafanulia Waislamu na wasiokuwa Waislamu kwamba njia ya ufumbuzi wa matatizo yote ya mwanadamu imo katika Qur’ani Tukufu.
Hassan al Mansuri amesema kuwa, Kituo cha Qur’ani cha haram ya Imamu Hussein AS kina zana za teknolojia ya kisasa kama komputa zinazotumiwa kufunza sheria na marifa ya Qur’ani na ratiba maalumu za mafunzo ya kusoma Qur’ani kwa njia sahihi kwa wanawake na wanaume.
Hasan al Mansuri amesema, kituo hicho kina mikakati ya kuanzisha masomo ya muda mfupi ya kusoma, kuhifadhi na sheria za tajwidi, kushirikiana na taasisi mbalimbali za Qur’ani nchini Iraq na kubadilishana uzoefu na tasisi hizo, kutayarisha mashindano ya Qur’ani na kuanzisha mtandao wa intaneti wa kituo hicho. 318223
captcha