Kwa mujibu wa ripota wa Shirika la Habari la Kimataifa la Quran (IQNA) katika mashindano hayo, Sayyid Mahdi Husseini kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ehsan Ashari mwakilishi wa Indonesia na Muhammad Amir Tawhidi kutoka Afghanistan kwa utaratibu, ndio waliochukua nafasi ya kwanza hadi tatu katika mashindano hayo.
Sayyid Mahdi Husseini alizaliwa mwaka 1983 katika mji wa kidini wa Qum nchini Iran na anasomea udaktari katika Chuo Kikuu Cha Masomo ya Tiba mjini Isfahan.
Ahmad Ashari ni mwanafunzi wa masomo ya kidini katika Chuo Kikuu cha Quran mjini Jakarta, Indonesia. Naye Muhammad Amir Tawhidi ana shahada ya kwanza katika masuala ya mawasiliano na anaendelea na masomo ya kidini katika Chuo Kikuu ya Kimataifa cha al Mustafa mjini Qum, Iran.
Huko nyuma Tauhidi alichukua nafasi ya tatu katika mashindano ya kwanza ya kimataifa ya wanachuo wa Kiislamu yaliyofanyika mjini Isfahan Iran, nafasi ya tatu katika mashindano ya kimataifa ya Quran ya Tehran na nafasi ya tatu katika mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Quran huko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Mbali na kutunukiwa nuskha ya Quran Tukufu na shahada ya kumbukumbu, washindi wa kwanza hadi wa tatu walipata $ 8000,
$ 6000 and $4000 kwa utaratibu.
Meya wa Mji wa Tehran Muhammad Baqir Qalibaf ni kati ya waliohudhuria sherehe za kuhitimisha mashindano hayo.
Makarii na Mahafidhi wa Quran kutoka zaidi ya nchi 40 walishiriki katika mashindano hayo yaliyofanyika kitika siku za Novemba 10-14 katika ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha mnara wa Milad mjini Tehran. 319996