Wazir ambaye amewakilisha Tanzania katika Mashindano ya Pili ya Kimataifa ya Qurani ya Wanachuo Waislamu ameliambia Shirika la Habari la Kimataifa la Qurani IQNA kuwa, anafurahia kuona wanawake wa Iran wanazingatia vazi la staha la Hijabu. Hata hivyo ameelezea masikitiko yake kuwa faradhi hii ya kidini (kuvaa Hijabu) haizingatiwi ni wanawake katika baadhi ya nchi za Kiislamu na Kiarabu na kusema hilo ni kinyume na mafunzo ya Qurani Tukufu.
Wazir ambaye ni mwanafunzi wa somo la udaktari katika Chuo Kikuu cha Muhimbili huko Dar-es-Salaam amesema kuwa mashindano ya Qurani ya wanachuo Waislamu ya Tehran yamekuwa fursa nzuri ya kukutana na wanachuo kutoka maeneo mbali mbali duniani na kubadilishana mawazo. Amesema, ameweza kupata maarifa zaidi alipokutana na makarii na mahafidhi wa Qurani ambao wanaendelea na masomo ya kawaida katika vyuo vikuu.
Akizungumzia uhusiano wa masomo yake ya udaktari na Qurani na dini amemuambia mwandishi wa IQNA kuwa, Mtume SAW amesema: 'Kila kila ugonjwa una dawa'. Amesema, katika somo la tiba kuna kitengo kiitwacho "Tiba ya Maimamu" ambacho kimetunikiwa kwa wanaadamu na Maimamu watukufu. Wazir amesema, usomaji Qurani unaathiri maisha ya mtu binafsi na ameashiria hadithi ya Mtume Muhammad SAW inayoema: "Kila mtu anayesoma Qurani, Maisha yake yatakuwa ya Qurani…"
Muhammad Wazir amesema, wananchi waliowengi Watanzania ni Waislamu na kuelezea masikitiko yake kuwa harakati za Qurani ni chache nchini humo.
Mwanachuo huyo wa Tanzania ametoa shukrani zake za dhati kwa watu wa Iran kutokana na ukarimu walioonyesha katika kipindi chote cha mashindano ya Qurani.
Makarii na Mahafidhi wa Qurani kutoka zaidi ya nchi 40 walishiriki katika mashindano hayo yaliyofanika kuanzia Novemba 10-14. 320016