IQNA

Fadhlullah akosoa uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa kwa Israel

11:01 - November 15, 2008
Habari ID: 1708281
Allama Muhammad Hussein Fadhlullah, mwanachuoni mashuhuri wa Lebanon amekosoa vikali uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa kwa utawala haramu wa Israel na kuulaumu kwa kuruhusu shughuli zake kudhibitiwa na Marekani.
Akizungumza na Machael Williams, mratibu maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na masuala ya Lebanon, Ayatullah Fadhlullah amechunguza matukio ya hivi karibuni yanayohusiana na askari wa kulinda amani wa umoja huo walioko nchini Lebanon, Unifil, na kusema kuwa inasikitisha kuwa utawala wa Israel umekuwa ukikiuka mara kwa mara mkataba nambari 1701 wa Umoja wa Mataifa bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria. Mar'ja huyo wa kidini ameashiria kutolaaniwa kwa jinai za Israel huko Qana na Umoja wa Mataifa, jinai ambazo zilitekelezwa na Shimon Peres katika kipindi cha ukatibu mkuu wa Boutros Ghali na kusikitishwa kwamba, umoja huo katika miaka ya hivi karibuni umekuwa ukidhibitiwa na Marekani kwa ajili ya kulinda maslahi yake haramu duniani. Huku akiashiria kushindwa umoja huo kuchukua hatua yoyote dhidi ya mashambulio ya kichokozi na ukiukaji wa anga ya Lebanon unaofanywa mara kwa mara na ndege za utawala ghasibu wa Israel, Allama Fadhlullah amesema kuwa jambo hilo linatekelezwa na Wazayuni kutokana na kushindwa Baraza la Usalama kuwachukulia hatua za kisheria. Ameseama, utawala wa Israel umemea pembe kutokana na uungaji mkono mkubwa wa Marekani kwake na pia udhibiti wa serikali ya Washington wa Baraza la Usalama. Amesisitiza kwamba hali hiyo ndiyo imeupelekea utawala haramu wa Israel kudumisha jinai zake za kinyama huko Palestina na kuendelea kuwazingira kutoka kila upande wakazi wa Ukanda wa Gaza. Allama Fadhlullah pia ameashiria kikao cha mazungumzo ya dini ambacho kimemaliza shughuli zake hivi karibuni huko New York Marekani na kuelezea masikitiko yake makubwa kutokana na uamuzi wa Umoja wa Mataifa kumualika mtenda jinai Sharon aketi kwenye meza moja na mataifa mengine yanayopigania haki na ukombozi wa mwanadamu. Amesema, Umoja wa Mataifa unakwenda kinyume kabisa na matakwa ya mataifa huru duniani kwa kushindwa kusimamisha ukiukaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na utawala ghasibu wa Israel, kushindwa kuufanya uondoke katika ardhi za Palestina na Lebanon, kubomoa ukuta wa kibaguzi na kusimamisha shughuli zake haramu za kuufanya mji mtukufu wa Quds kuwa wa Kiyahudi. 320123
captcha