Sherehe za kufunga mashindano hayo zilihudhuriwa na Meya wa jiji la Tehran, Muhammad Baqir Qalibaf, Mahdi Chamran Mkuu wa Baraza la Kiislamu la Mji wa Tehran, Rahim Khaki Mkuu wa Jumuiya ya Qur'ani ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Iran, wabunge na shakhsia wengine wa kisiasa na kidini.
Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanafunzi Waislamu wa Vyuo Vikuu yalianza tarehe 10 mwezi huu wa Novemba katika ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Milad na yalimalizika jioni ya jana kwa kutangazwa washindi wa mashindano hayo. 320044