Hayo yamesemwa na Hussein Sabzali ambaye alishiriki kama karii katika mashindano ya pili ya kimataifa ya Quran ya wanachuo yaliyomalizika hivi karibuni mjini Tehran. Katika mahojiano na Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani amesema kuwa kufanyika mashindano ya Quran ya wanachuo kunaandaa mazingira ya wasomi na wataalamu wa Qur'ani kutoka nchi za Kiislamu kukutana mahala pamoja na kutumia nguvu za ujana katika njia ya kueneza utamaduni halisi wa Kiislamu.
Ameongeza kuwa: 'Kufanyika mashindano ya kimataifa ya Quran Tukufu ya wanachuo ni jambo la dharura kwani huwasaidia wanachuo kufahamu kwa kina cha maana ya kitabu hiki cha Mwenyezi Mungu.
Karii huyo wa kimataifa wa Qur'ani kutoka Iran ameashiria nafasi ya mashindano hayo katika kuleta umoja miongoni mwa Waislamu na kuongeza kuwa: ' hakuna shaka kwamba kukutana pamoja vijana kutoka nchi za Kiislamu ambao ni wafuasi wa madhehebu mbali mbali kutawasaidia kuelewana na kufahamiana. Amesema, hili litaimarisha moyo wa ukuruba miongoni mwa vijana wa Kiislamu.
Sabzali amemaliza kwa kuashiria kuenziwa mabingwa wa Qur'ani katika ulimwengu wa Kiislamu kama vile Ustadh Abul Einein Sheisha wa Misri katika mashindano hayo na kusema: 'Ustadh Sheisha ni kati ya makarii wa zama za dhahabu nchini Misri na kuenziwa kwake katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutambakishia kumbukumbu za kudumu kuhusu Iran"
Makarii na Mahafidhi wa Quran kutoka zaidi ya nchi 40 walishiriki katika mashindano hayo yaliyofanyika kitika siku za Novemba 10-14 katika ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha mnara wa Milad mjini Tehran.
317536