IQNA

Qurani, kigezo cha kukabiliana na fitna

12:11 - November 16, 2008
Habari ID: 1708667
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria aya ya 103 ya sura Al Imran katika Quran Tukufu isemayo, "Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane." na kusema kuwa mwito wa Umoja unapaswa kuwa juu ya msingi wa ukweli na mafunzo ya Qurani Tukufu.
Hii ndio njia muafaka kwa Waislamu kukabiliana na fitina zinazoenezwa na madola makubwa ya kibeberu.
Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah Sheikh Naim Qasim amenukuliwa na gazeti la kila siku la Lebanon la Al Annahar akisema hayo alipokutana na ujumbe wa Jumuiya ya Umoja wa Kiislamu huko Lebanon unaoongozwa na Dr. Kamal Helbawi ambaye ni Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo. Sheikh Qasim ameelezea furaha yake kukutana na ujumbe huo hasa katika kipindi hiki ambacho maadui wanapanga njama za kuzusha mifarakano miongoni mwa Waislamu.
Kiongozi huyo mwandamizi wa harakati ya Hizbullah amesema, kinyume na kuzusha mifarakano ambako kunahitajia mipango na njama maalumumu, kuwaita watu kwa lengo la kuleta umoja miongoni mwa Waislamu hakuhitaji jitihada ngumu kwa sababu Waislamu kimaumbele wako katika mkondo wa umoja.
Sheikh Naim Qasim amebainisha kuwa 'leo hii tunatumia nguvu zetu zote katika kukabiliana na uvamizi wa Israel pamoja na njama za maadui wa kigeni za kuwa na satwa katika nchi yetu na kwa sababu ya mustaqabali wa vijana wetu tutaendelea na azma yetu ya kusimama kidete'. 320204

captcha