IQNA

Hali ya Waislamu Balkan yatathminiwa

11:55 - November 16, 2008
Habari ID: 1708668
Kongamano la kimataifa chini ya anuani ya : "Uislamu kusini-mashariki mwa Ulaya" limefanyika mjini Berlin, Ujerumani kwa lengo la kutathmini hali ya Waislamu katika eneo la Balkan.
Kwa mujibu wa ripota wa Shirika la Kimataifa la Habari za Quran (IQNA) huko Balkan, kongamano hilo limewashirikisha wawakilishi kutoka Bulgaria, Bosnia Herzegovina , Albania, Macedonia, Kosovo na Ugiriki.
Kwa mujibu wa duru katika kongamano hilo, washiriki walijadili suala nyeti kuhusu iwapo kuna 'Uislamu wa Balkan' au la katika eneo la kusini-mashariki mwa Ulaya.
Baadhi ya wataalamu wa masuala ya utamaduni ya Balkan, ambao wengi wao si Waislamu, wanatoa nadharia kuwa eti kuna "Uislamu wa Balkan" katika eneo hilo! Hii ni katika hali ambayo wengi wa wataalamu wa kidini ambao ni Waislamu wanaamini kuwa katika eneo la Balkan kuna aina maalumu ya utamaduni wa Kiislamu na si aina mpya ya Uislamu kama inavyodaiwa.
320287

captcha