IQNA

Kitengo cha wanawake chaongezwa mashindano ya kimataifa ya Qurani ya vijana huko Qatar

12:43 - November 16, 2008
Habari ID: 1708744
Mwenyekiti wa Idara ya Masuala ya Vijana ya Qatar Khalid Yusuf al Mulla amesema kuwa kitengo cha wanawake kimeongezwa katika Mashindano ya 21 ya Kimataifa ya Quran na Hadithi ya vijana wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Ghuba ya Uajemi.
Khalid bin Yusuf amesema, uamuzi wa kuwashirikisha wanawake katika mashindano hayo umechukuliwa kufuatia pendekezo lililotolewa na Qatar kwa Mawaziri wa Vijana na Michezo wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushikiano wa Ghuba ya Uajemi. Ameongeza kuwa juhudi zinafanyika kuhakikisha kwamba mashindano hayo yanayodhaminiwa na serikali ya Qatar yanafanyika kwa mafanikio.
Khalid Yusuf al Mulla amesema, Mashindano ya 21 ya Qur’ani na Hadithi ya Vijana ambayo yataanza tarehe 20 mwezi huu wa Novemba yatawashirikisha wawakilishi wa nchi za Qatar, Saudi Arbia, Imarati, Kuwait, Bahrain na Oman.
Mashindano hayo yatakayoendelea kwa kipindi cha siku tano yatahusisha kuhifadhi, kusoma, tajwidi ya Qur’ani pamoja na kuhifadhi hadithi za Mtume Muhammad SAW. Washindani wanalazimika kuhifadhi sura za Yunus na Hud na kusoma sura za Maryam, Twaha, Anbiyaa, Haj na Muuminun na kuhifadhi hadithi 37 za Mtume kutoka kitabu cha Riyadhu al Swalihin cha Nawawi. 320511
captcha