Lengo la hati hiyo limetajwa kuwa ni kuimarisha amani na utaratibu ulimwenguni kwa shabaha ya kuarifisha masuala ya pamoja kati ya dini tofauti. Wafuasi wa dini mbalimbali pia wamealikwa kutoa maoni yao kuhusiana na jinsi ya kubuniwa na kuandikwa hati hiyo katika tovuti iliyotajwa. Baada ya kutayarishwa, hati hiyo itatiwa saini na viongozi kadhaa wa kidini. Tovuti ya Charterforcompassion.org imezinduliwa na Carrel Armstrong, mtaalamu mashuhuri wa masuala ya kidini wa Marekani. Ameandika vitabu 30 kuhusiana na masuala ya pamoja yanayowashirikisha wafuasi wa dini tofauti. Anaandika katika tovuti hiyo kwamba, katika dunia ya leo, walimwengu wana jukumu la kubuni jamii ambayo watu wote wataweza kuishi pamoja kwa amani na utulivu bila ya kujali dini na itikadi zao. 321049