Idara inayosimamia masuala ya kiutamaduni ya Wairani waishio nje ya nchi katika taasisi hiyo imetangaza kuwa, CD hizo maalumu imetayarishwa ili kuhimiza utamaduni wa Qur'ani na vile vile kutokana na udharura wa kuhakikisha Wairani waishio nje ya nchi yao wanadumisha utambulisho wao wa Kiislamu.
CD hizo nne zina tafsiri za Kifarsi na Kiingereza za Quran Tukufu pamoja na mfumo wa sauti wa Dolby.
Taasisi ya Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu vile vile inajihusisha na harakati nyinginezo za kusambaza fikra za Kiislamu duniani. Taasisi hiyo ina ofisi katika nchi 60 na imekuwa ikitawanya CD za kidini na Qur'ain kote ulimwenguni. 321648