Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mtandao wa intaneti wa eshia ambao ulianzishwa kwa ajili ya kusahilisha mawasiliano kati ya wananchi na Marajii (wanazuoni wa ngazi za juu kabisa wa kidini) na wataalamu wa masuala ya Kiislamu, sasa unatangaza moja kwa moja masomo ya usooli na fiqhi ya Ayatullah Jazairi anayefunza katika chuo cha kidini cha Ahwaz.
Masomo ya Usooli ya Ayatullah Jazairi yanaanza saa nne na nusu hadi tano na robo kwa saa za Iran nayo masomo ya fiqhi huanza saa moja hadi mbili kasorobo vile vile kwa saa za Iran.
Kituo hicho cha kidini pia kinatangaza kupitia intaneti masomo ya Ayatullah Mazaheri na marajii wengine ambao ni Ayatullah Makarim Shirazi, Ayatullah Nuri Hamedani, Ayatullah Subhani na masomo ya tafsiri ya ya Qurani Ayatullah Jawad Amoli.
Aidha kusahilisha mawasiliano kati ya Mashia na Maulama wa kidini katika kujibu masuala ya kisheria na kifiqhi ni kati ya malengo mengine ya mtandao huo. Anuani ya mtandao huo ni http://www.eshia.ir
321772