IQNA

Hatua ya France Press ya kueneza uongo dhidi ya Uislamu

10:57 - November 18, 2008
Habari ID: 1709573
Shirika rasmi la habari la Ufaransa, France Press limechukua hatua ya kukabiliana na Uislamu na mafundisho yake yenye thamani kubwa kwa kueneza uongo na madai yasiyo na msingi huko Kosovo. Shirika hilo la Ufaransa lemedai kuwa vijana wa Kiislamu wa Kosovo wanapenda sana kuiga tabia za vijana wenzao wa nchi za Ulaya.
Limesema vijana hao wa Kiislamu hupenda kuiga mitindo ya mavazi ya vijana wa Ulaya na pia kujishughulisha na masuala ya starehe nje ya nyumba zao hadi usiku wa manane. Limeendelea kusema kuwa, vijana hao hunywa pombe na wala hawapendi kujishughulisha na masuala ya kidini. Shirika hilo pia limefanya mahojiano na wahadhiri kadhaa wa vyuo vikuu ambao wamedai kuwa ni jamo la kawaida kwa Wakosovo kufungamana na utamaduni na tabia za nchi za Magharibi kwa sababu ni Marekani na Ulaya ndizo zilizoikomboa Kosovo. Huku likiashiria idadi kubwa ya Waislamu nchini Kosovo, shirika hilo la habari limesema kuwa adhana zinazoadhiniwa kupitia minara ya makumi ya misikiti ya mji mkuu Prishtina, haziwashughulishi vijana wa nchi hiyo. Matukio ambayo yamekuwa yakiwakumba Waislamu wa nchi za Balkan yamekuwa yakizingatiwa sana na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi na Waislamu wa nchi nyinginezo, kutokana na mivutano ya kikabila na kidini ambayo imekuwa ikitokea katika eneo hilo. Baadhi ya vyombo vya habari vya Magharibi vimekuwa vikifuatilia masuala ya kuzusha chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu katika eneo hilo. Hii ni katika hali ambayo wanazuoni wa maeneo kama vile Bosnia Herzegovina, Kosovo na Prishtina wanasema kuwa maeneo hayo ni mstari wa mbele wa Uislamu barani Ulaya na kwamba wanafuatilia kwa karibu matukio ambayo yanapelekea kuongezeka kwa idadi ya Waislamu katika eneo hilo. Idadi kubwa ya watu milioni mbili wa Kosovo ni Waislamu na katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni misikiti na vituo vya utamaduni vya Kiislamu vimekuwa vikiongezeka katika nchi hiyo. Jambo hilo pekee linathibisha hamu kubwa ya Waislamu wa Kosovo ya kufungamana na thamani za dini yao tukufu ya Kiislamu. 321316
captcha