IQNA

Kufeli kwa kikao cha mazungumzo ya kidini mjini New York

10:11 - November 19, 2008
Habari ID: 1710063
Sayyid Hassan an-Namr, mwanafikra wa Kishia wa nchini Saudi Arabia amesema kuwa kikao kilichoandaliwa hivi karibuni na Umoja wa Mataifa huko New York kwa wito wa Saudi Arabia, hakikuwa na natija yoyote ya maana katika kuleta amani, uadilifu na usalama ulimwenguni.
Akiashirikia kikao hicho cha mazungumzo ya kidini mjini New York, Sayyid Hassan an-Namr amesema kuwa, mazungumzo kama hayo yanapasa kufanyika katika msingi wa sheria za Mwenyezi Mungu na kwa lengo la kuleta amani, uadilifu na usalama duniani. Msomi na mwandishi huyo wa Kishia ameendelea kusema kuwa, kuhudhuria Shimon Peres, rais wa utawala haramu wa Israel katika kikao hicho, ni jambo lililowashangaza wengi duniani na kukifanya kuwa kikao cha kawaida tu cha kisiasa ambacho kiko mbali kabisa na malengo ya mazungumzo ya kidini na ustaarabu wa ulimwengu. Mwanafikra huyo ambaye pia ni Imam wa Msikiti wa Hamza wa mjini Saihat amesema, kikao cha mazungumzo ya kidini kinapasa kuwajumuisha wanafikra wa Kiyahudi, Kiislamu na Kikristo tu ambao wanafahamu vyema misingi ya dini za mbinguni na sio wanasiasa katili wasiokuwa na ufahamu wowote kuhusiana na thamani za kidini wala kiutu. Kuhudhuria Peres katika kikao hicho kulikabiliwa na ukosoaji mkubwa wa wanafikra na wanazuoni wa nchi za Kiislamu na Kiarabu. 322166
captcha