Warsha hiyo inasimamiwa na Wizara ya Hija ya Saudi Arabia.
IQNA imenukuu gazeti la al Riyadh kwamba Waziri wa Hija wa Saudi Arabia Fouad bin Abdulsalam al Farsi amesema, katika warsha hiyo kutatolewa mafunzo juu ya namna ya kupita makundi ya mahujaji juu ya daraja la Jamarat na ibada ya kupiga mawe nembo za mashetani.
al Farsi amesema kuwa wataalamu wanaoshiriki katika warsha hiyo pia watawasilisha makala kuhusu "Matukio ya ibada ya hija katika mwaka 1429 Hijria", Mpango wa kuondoka mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kupiga mawe shetani", Mchango wa takwimu na tarakimu katika uratibu sahihi wa ibada ya hija" na Mabadiliko ya kihandisi na kiujenzi ya daraja la Jamarat."
Waziri wa Hija wa Saudia ameongeza kuwa wizara yake imebuni mipango ya kuratibu na kusimamia harakati za mahujaji juu ya daraja la Jamarat katika ibada ya hija. 322219