IQNA

Wizara ya Hija Saudia yazindua mtandao wa Intaneti

12:51 - November 20, 2008
Habari ID: 1710458
Mtandao wa intaneti wa Wizara ya Hija ya Saudi Arabia umezinduliwa kwa lengo la kutoa huduma kwa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu (Baitullah al Haram)
Jarida la Saudi Gazette limeripoti kuwa, mtandao huo wenye anwani ifuatayo www.localhajj.info , una habari zote kuhusu mashirika yanayotoa huduma kwa mahujaju wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa lugha ya Kiarabu.
Aidha mtandao huo wa intaneti una habari za fiqhi na amali za hija pamoja na ramani ya maeneo mbali mbali matakatifu. 322871

captcha