IQNA

Kozi mjini Karbala yalenga kuimarisha ujuzi wa majaji wa mashindano ya Qur’ani

17:05 - July 28, 2026
Habari ID: 3482547
k
IQNA - Kozi ya Qur’ani imefanyika mjini Karbala, Iraq, kwa lengo la kuimarisha ujuzi wa majaji wanawake wa mashindano ya Qur’ani.

Kwa mujibu wa ripoti ya Al-Kafeel, kozi hiyo iliandaliwa na Idara ya Masomo ya Qur’ani ya Fatima bint Asad, iliyo chini ya Idara ya Masuala ya Wanawake katika Haram Tukufu ya Hadhrat Abbas (AS).

Lengo la kozi hiyo lilikuwa ni kukuza ujuzi wa kitaaluma na kuwanoa majaji wanawake kwa ajili ya mashindano ya Qur’ani. Kozi hiyo ilijikita katika kuimarisha uwezo wa uhakiki na tathmini, pamoja na kuongeza ufanisi wa utendaji katika nyanja za upangaji, utekelezaji na mbinu za uamuzi.

Lengo jingine la kozi hii lilikuwa ni kujitahidi kufikia matokeo bora zaidi katika mchakato wa kufundisha shughuli za Qur’ani na programu za kielimu zinazoandaliwa na idara hiyo katika kipindi chote cha mwaka.

Mpango huo ulifanyika kwa muda wa siku mbili, kwa vipindi vya saa tatu kila siku, katika makao makuu ya Idara ya Masomo ya Qur’ani ya Fatima bint Asad. Kozi hiyo ilijumuisha mbinu za kisasa za ufundishaji pamoja na mazoezi mbalimbali ya mtu mmoja mmoja na ya vikundi.

Programu za kozi hiyo pia zililenga kuwawezesha washiriki katika matumizi ya mikakati iliyoidhinishwa ya uhakiki na uamuzi, kupitia muunganiko wa umilisi, mwingiliano na mafunzo ya kiujuzi.

Kozi hiyo ilihitimishwa kwa mazoezi ya vitendo na mitihani ya maandishi iliyojengwa juu ya kanuni zilizowekwa kwa namna ya pamoja na zilizoidhinishwa kitaifa, kwa lengo la kutathmini kiwango cha ufaidikaji wa washiriki kutokana na mada za mafunzo, kuimarisha maudhui yaliyowasilishwa katika fikra za washiriki, na kuhakikisha utekelezaji wake wa kivitendo katika shughuli zijazo.

Kupitia kozi kama hizi, Idara ya Masomo ya Qur’ani ya Fatima bint Asad inalenga kuwawezesha watumishi wa Qur’ani, kuongeza ufanisi wa utendaji wao katika uhakiki wa mashindano, na kuwajengea uwezo katika huduma kwa Qur’ani Tukufu kwa mujibu wa viwango vya juu zaidi vya kitaaluma na kielimu.

3498436

Habari zinazohusiana
Kishikizo: karbala qurani tukufu
captcha