IQNA

17:09 - July 29, 2026
Habari ID: 3482555

Washindani 82 wa nchi 33 washiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu Qatar

IQNA – Hatua ya mchujo ya Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya “Awali wa Waliotangulia” (First of the Firsts) imezinduliwa nchini Qatar.

q

Mashindano hayo yamekusanya kundi la maqari wateule na mahafidh wa Qur’ani Tukufu kutoka kote ulimwenguni.

Jumla ya washindani 82 kutoka nchi 33, ambao wote ni washindi wa kwanza katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani wanashiriki katika duru za mchujo za siku tano kwa njia ya mtandao, zinazoendelea hadi tarehe 30 Julai.

Mashindano haya yameandaliwa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar chini ya mwavuli wa Mashindano ya Qur’ani Tukufu ya Sheikh Jassim bin Mohammed bin Thani.

Kwa mujibu wa waandaaji, tukio hili adhimu linaonyesha mchango mkubwa wa Qatar katika kuitumikia Qur’ani Tukufu, kuwaunga mkono mahafidh wake, na kuimarisha maadili pamoja na utambulisho wa Kiislamu.

3498446

Habari zinazohusiana
captcha