Kwa mujibu wa tangazo hilo, mkoa wa Karbala utafungwa rasmi kuanzia Jumatano hadi Jumatatu ili kuwezesha maandalizi na huduma zinazofaa kwa mazuwari wa Arbaeen.
Wakati huo huo, siku ya Arbaeen inapokaribia, Kituo cha Habari za Usalama cha Iraq kimewataka mazuwari wa Arbaeen kutumia usafiri wa umma badala ya magari binafsi.
Katika taarifa iliyochapishwa na Shirika Rasmi la Habari la Iraq (INA), kituo hicho kimewaalika mazuwari kutumia vyombo vya usafiri wa umma.
Kituo hicho pia kimeielekeza idara ya trafiki nchini humo kuongeza ufuatiliaji wa utekelezaji wa hatua za usalama na salama, hasa wakati halijoto inapozidi kuongezeka.
Arbaeen ni munasaba wa kidini unaoadhimishwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia katika siku ya arobaini baada ya Ashura, kwa kumbukumbu ya shahada ya Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na Imamu wa tatu katika madhehebu ya Shia.
Ni miongoni mwa ziara kubwa zaidi za kidini kila mwaka duniani, ambapo mamilioni ya Waislamu wa Shia, pamoja na wengi miongoni mwa Sunni na wafuasi wa dini nyingine, hutembea kwa miguu kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arbaeen itaangukia tarehe 4 Agosti.
3498442