Sheria hiyo ilisainiwa na Rais wa Ireland, Catherine Connolly, na kukamilisha taratibu zote za kikatiba zinazohitajika ili kuanza kutumika rasmi.
Wizara hiyo imeeleza kuwa hatua hiyo ni hatua muhimu inayoendana na juhudi za kidiplomasia za Palestina za kukata vyanzo vya usaidizi kwa miradi haramu ya ujenzi wa vitongoji vya utawala haramu wa Israel, na inaakisi dhamira ya Ireland katika kuheshimu misingi ya sheria za kimataifa na uadilifu wa kiulimwengu.
Imesisitizwa kuwa, utekelezaji wa sheria za kimataifa ni wajibu wa kisheria unaoyataka mataifa kutotambua au kutosaidia hali isiyo ya kisheria iliyosababishwa na uvamizi wa Kizayuni na shughuli zake za ujenzi wa vitongoji, ikijumuisha kupitia shughuli za kibiashara, kiuchumi, kifedha, uwekezaji na huduma zinazohusiana na vitongoji hivyo haramu.
Wizara hiyo pia imetoa wito kwa nchi, mabunge na watunga sheria kote ulimwenguni kufuata mfano wa Ireland kwa kuimarisha mifumo ya uwajibikaji ya kimataifa na kuweka vikwazo dhidi ya miradi haramu ya ujenzi wa vitongoji ya utawala wa Kizayuni, wavamizi wa Kiisraeli, na kile ilichokitaja kama makundi yao ya kigaidi.
Sheria hiyo imeanza kutumika rasmi baada ya kusainiwa na Rais Connolly mnamo tarehe 23 Julai, kufuatia kuidhinishwa kwake na bunge la wawakilishi mnamo tarehe 7 Julai na baraza la seneti mnamo tarehe 15 Julai.
3498426