Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Khabrein, Frederic Desagneaux Naibu Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa ametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa: "Serikali ya Ufaransa imechapisha vitabu 50 elfu vya kuwaongoza mahujaji Wafaransa katika kutekeleza amali zao za hija".
Amesema Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa inashirikiana na wizara kadhaa pamoja na jumuiya za Kiislamu nchini humo ili kuhakikisha mahujaji Wafaransa wanatekeleza amali za hija bila matatizo.
Frederic Desagneaux amesisitiza kuwa wakuu wa Ufaransa watafanya kila wawezali kutoa huduma bora kwa mahujaji wa nchi hiyo katika muda wote watakaokuwa Saudi Arabia kwa ajili ya ibada ya hija. 322883