Habari katika mtandao huo wa Islamonline zinasema kuwa, mafunzo kupitia intaneti kwa ajili ya mahujaji kwa lugha za Kiarabu na Kiingereza yanafanyika chini ya usimamizi wa kitengo cha Sheria za Kiislamu cha mtandao huo wa intaneti.
Katika programu hiyo, kuna taswira za muongozo wa misingi yote ya hija na hatua zote za ibada hiyo zimebainishwa kwa taratibu.
Safari ya kwanza ya kiintaneti ya hija katika mtandao wa Islamonline ilifanyika kwa lugha ya Kiingereza tarehe 19 Novemba.
Programu hiyo ilitayarishwa kwa muda wa masaa 150 na wataalamu watatu wa programu za kompyuta kutoka Saudi Arabia. 322850