IQNA

Kikao cha kimataifa cha 'Mazungumzo ya Kidini, Ukweli na Mustakbali' Nchini Libya

12:41 - November 20, 2008
Habari ID: 1710462
Kikao cha siku mbili cha 'Mazungumzo ya Kidini, Ukweli na Mustakbali' kilimaliza shughuli zake jana huko Tripoli, mji mkuu wa Libya ambapo wasomi na wanafikra kutoka nchi hiyo, Misri na Syria walishiriki.
Katika kikao hicho kilichoandaliwa na Taasisi ya Wakfu ya Libya, washiriki walijadili na kubadilishana mawazo kuhusian ana uhakika, mustakbali na udharura wa kufanyika mazungumzo ya kidini na vilevile nafasi ya taasisi za kidinika katika kueneza mafundisho halisi ya dini tukufu ya Kiislamu. Wasomi na wanafikra wa Kiislamu walioshiriki katika kikao hicho vilevile walichunguza pande tofauti za mazungumzo ya kidini na nafasi ya taasisi za kidini katika kueneza mafundisho ya kidini, matatizo na changamoto, namna ya kutumia teknolojia mpya katika kuhubiri Uislamu katika ulimwengu wa leo na tofauti zilizopo kuhusiana na ukweli wa Uislamu na njia zinazotumika katika kuihubiri dini hii tukufu ya Mwenyezi Mungu. 322729
captcha